Matthew 22:15-22

Kulipa Kodi Kwa Kaisari

(Marko 12:13-17; Luka 20:20-26)

15 aNdipo Mafarisayo wakatoka nje wakaandaa mpango wa kumtega Yesu katika maneno yake. 16 bWakatuma wanafunzi wao kwake pamoja na Maherode. Nao wakasema, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonyesha upendeleo. 17 cTuambie basi, wewe unaonaje? Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”

18Lakini Yesu, akijua makusudi yao mabaya, akawaambia, “Enyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? 19Nionyesheni hiyo sarafu inayotumika kwa kulipia kodi.” Wakamletea dinari. 20Naye akawauliza, “Sura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?”

21 dWakamjibu, “Ni vya Kaisari.”

Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”

22 eWaliposikia hili, wakashangaa. Hivyo wakamwacha, wakaenda zao.

Copyright information for SwhNEN